Swali: Ndugu yangu amepatwa na ugonjwa wa ukurutu. Ni lazima kuosha viungo vyake vilivyopatwa na ukurutu? Au anaweza kufanya Tayammum kwa sababu uoshaji unamcheleweshea kupona?

Jibu: Ikiwa kuosha kwa maji kunamuathiri na kumzidishia maradhi, asioshe na badala yake afanye Tayammum. Aoshe vile viungo visivyogonjweka na afanye Tayammum kwa vilivyogonjweka.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (69) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/12-07-1438i.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2017