Ugomvi wa majirani juu ya eneo linaloshukiwa kuwa na makaburi


Swali:

السلام عليكم و رحمة الله و بركاته

Namiliki ardhi pambizoni na mali za wengine. Ardhi hiyo, ambayo hapo kitambo ilikuwa na marundo ya changarawe, nimehuisha miti ya tamariski kwa karibu sasa miaka 43. Kwa kuongezea, nina hati na vibali kutoka kwa manispaa ya ujenzi ya kujengea katika ardhi hiyo. Lakini kumejitokeza kikosi cha watu wanaonipinga kujengea juu yake kwa hoja kwamba ardhi hiyo iko na makaburi mengi. Hao wapinzani ni majirani zangu na punde kidogo ndio wamenunua ardhi zao. Wameamua kununua ardhi hiyo kutoka kwangu, lakini nimekataa kwa sababu nataka kujenga jengo la kuishi ndani yake. Nimechimba ardhi hiyo ili nione kama kuna athari yoyote ya makaburi, lakini sikuona athari yoyote inayoonyesha kuwa kuna makaburi. Je, niendelee kuishi hapo au niachane nayo?

Jibu:

بسم الله الرحمن الرحيم

و عليكم السلام و رحمة الله و بركاته

Kama umechimba ardhi kwa kina kabisa kwa kiasi cha kwamba kama kungelikuwa kuna makaburi basi yangelionekana, basi hakuna neno kwako kujenga nyumba ya kuishi muda wa kuwa hakujathibiti kuwa ardhi hiyo iko na makaburi.

1399-11-12

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/195)
  • Imechapishwa: 01/07/2021