Ufafanuzi juu ya mapokezi mengi yaliyopokelewa juu ya swalah ya kupatwa kwa jua


Swali: Kumepokelewa juu ya swalah ya kupatwa kwa jua sifa mbalimbali pamoja na kuwa hakukupatwa kwa jua kipindi cha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) isipokuwa mara moja tu. Ni vipi tutaoanisha kati ya Hadiyth hizi?

Jibu: Wanachuoni wahakiki, kama mfano wa al-Bukhaariy na wengineo, wanaona kuwa Sunnah katika swalah ya kupatwa kwa jua ni Rakaa´ mbili ambapo katika kila Rakaa´ kuna Rukuu´ mbili na Sujuud mbili. Haya ndio walioafikiana kwayo mashaykh wawili; al-Bukhaariy na Muslim. Kumepokelewa vilevile katika “as-Swahiyh” ya Muslim nyongeza badala ya Rukuu´ mbili zikawa tatu, nne na tano. Wanachuoni wahakiki wanaonelea kuwa yenye kuzidi juu ya Rukuu´ mbili inazingatiwa kuwa ni Hadiyth dhaifu. Hayatakiwi kutendewa kazi. Pamoja na kuwa kuna wanachuoni wengine wanaonelea kuwa yanatakiwa kutendewa kazi na wakasema kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliishi al-Madiynah miaka kumi na kwamba kuna uwezekano kwamba jua lilipatwa mara nyingi. Kujengea juu ya hili wanaonelea kuwa hakuna neno. Wamefasiri hili kwamba jua linaweza kuwa lilipatwa mara nyingi. Kujengea juu ya hili wanaona kuwa ni sawa na wamefasiri kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuna wakati aliswali katika kila Rakaa´ Rukuu´ mbili, mara nyingine katika kila Rakaa´ aliswali Rukuu´ tatu, wakati mwingine Rukuu´ nne na wakati mwingine Rukuu´ tano.

Lakini pamoja na haya yote wanachuoni wahakiki wanaonelea kuwa chenye kutegemewa ni Rakaa´ mbili na kwamba katika kila Rakaa´ kuna Rukuu´ mbili na Sujuud mbili. Mengineyo wanaoenelea kuwa ni dhaifu.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (02) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/429/429.mp3
  • Imechapishwa: 07/03/2018