3- Ahmad amepinga kushabihisha (التشبيه). Hanbal amesema kwamba amesema:

“Mshabihishaji anasema uoni [wa Allaah] ni kama uoni wangu, mkono [wa Allaah] ni kama mkono wangu na unyayo [wa Allaah] ni kama uoni wangu. Mwenye kusema hivo basi amemshabihisha Allaah na viumbe Wake.”

4- Amesema katika upokezi wa Yusuuf bin Muusa:

لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖوَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ

“Hakuna chochote kinachofanana Naye – Naye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.”[1]

Haijuzu kutumia Hadiyth ya Abu Hurayrah kwa wale wanaothibitisha sifa. Kwa sababu Allaah sehemu nyingi katika Qur-aan amejisifu Mwenyewe, Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pia amefanya hivo katika Hadiyth ambazo ni Swahiyh na vilevile Salaf wa Ummah huu wakafanya hivo, kama tutakavyobainisha huko mbele. Kwa hivyo Hadiyth inaweza kutumiwa kwa wale wanaozungumzia Allaah kwa njia isiyokuwa na dalili katika Shari´ah.

Tambua ya kwamba haijuzu kuzirudisha Hadiyth hizi kama walivyopita Mu´tazilah wala kuzifasiri kwa kuzipindisha maana kama walivyofanya Ashaa´irah. Lililo la wajibu ni kuziamini kwa udhahiri wake na kwamba ni sifa za Allaah zisizofanana na sifa za viumbe. Wala hatuonelei kuwa zinafanana na sifa za viumbe Wake. Lakini tunachosema juu ya Hadiyth hzi ni yale yaliyosemwa na Shaykh na imamu wetu Abu ´Abdillaah Ahmad bin Muhammad bin Hanbal na maimamu wengine wa Ahl-ul-Hadiyth:

“Zipitsheni kama zilivyokuja.”

Kwa hivyo zinatakiwa kufahamika kwa udhahiri wake kwa sababu ni sifa za Allaah (Ta´ala) zisizofanana na sifa za viumbe.

[1] 42:11

  • Mhusika: Imaam Abu Ya´laa Muhammad bin al-Husayn al-Farraa’
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ibtwaal-ut-Ta’wiyl (1/43-44)
  • Imechapishwa: 21/12/2018