Tofauti ya makafiri na waislamu kwa mama zao

Swali: Ni ipi hukumu ya kusherehekea siku ya mama na kupeana zawadi? Baadhi ya watu wakati ninapowaambia kuwa jambo hili halifai wanasema tusiwe na msimamo mkali.

Jibu: Haya ni matendo ya makafiri. Sikukuu hii inamnufaisha nini mama? Haimnufaishi kitu. Kinachomnufaisha ni kumtendea wema na kumuombea du´aa. Haya ndio yenye kumnufaisha. Ama kusherehekea sikukuu hii haimnufaishi kitu na isitoshe ni haramu. Ni kujifananisha na makafiri. Makafiri wao hawawatambui mama zao isipokuwa siku ya sikukuu. Muislamu yeye anamtambua mama yake katika kila wakati na kila siku, ni mamoja wakati anapokuwa yuhai au ameshakufa. Anamtambua, anamkumbuka na anamuombea du´aa. Ama wao hawawatambuki mama zao isipokuwa siku ya sikukuu hii.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (66) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-04-16.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020