Ujuu (´Uluw) ni sifa miongoni mwa sifa za Allaah. Kulingana (Istiwaa´) ni sifa miongoni mwa sifa za Allaah. Kuna tofauti gani kati ya sifa hizo mbili? Tofauti inabainika wazi wazi kati ya sifa hizi mbili kwa njia mbili:

1- Ujuu ni katika sifa za dhati na hivyo inakuwa ni yenye kulazimiana na Mola. Mola hawi isipokuwa kwa juu.

Kulingana ni katika sifa za kimatendo na amefanya hivo baada ya kuumba mbingu na ardhi. Hivyo ndivyo alivyosema Allaah katika Kitabu Chake. Hiyo ikawa ni dalili yenye kuonesha kuwa wakati fulani alikuwa ni mwenye kulingana juu ya ´Arshi na wakati mwingine alikuwa si mwenye kulingana katika ´Arshi. Kulingana juu ya ´Arshi ni jambo lililokuwa baada ya kuumba mbingu na ardhi. Kulingana ni uwepo juu maalum. Kila mwenye kulingana juu ya kitu anakuwa juu yake, na si kila ambaye anakuwa juu ya kitu anakuwa ni mwenye kulingana juu yake.

Asli ni kwamba uwepo juu Wake (Subhaanah) ni sifa inayolazimiana na Yeye kama jinsi Ukubwa Wake, kustahiki Kwake kiburi na uwezo Wake ni vyenye kulazimiana Naye. Ama kuhusiana na kulingana ni kitendo anachokifanya (Subhaanah) kwa matakwa Yake na Uwezo Wake. Kwa ajili hii ndio maana amesema:

ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ

“… kisha akalingana juu ya ´Arshi.” (07:54)

2- Uwepo juu ni miongoni mwa sifa zenye kujulikana kwa dalili za Kishari´ah na kwa akili pia. Ama kulingana ni miongoni mwa sifa zenye kujulikana kwa dalili za Kishari´ah na si kwa akili. Ninachotaka kusema ni kwamba, watu wote wanathibitisha na kujua kuwa Allaah yuko kwa juu. Mpaka wanyama wanajua hili. Ama kuhusiana na kulingana juu ya ´Arshi, hili halikujulikana isipokuwa kupitia njia ya Shari´ah.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (01/400-401)
  • Imechapishwa: 19/05/2020