Tofauti ya kuchemua na salamu katika kurudisha

Swali 201: Mwenye kupiga chafya na akamhimidi Allaah ni lazima kwa yule mwenye kumsikia kumuitikia?

Jibu: Ni lazima na sio kama salamu ambapo anatosha mmoja wakati anapotusalimia “as-Salaam ´alaykum” mmoja wetu anaweza kusema “wa ´alaykumus-Salaam”. Kuhusu kuchemua ni haki kwa mwenye kumsikia kumtakia rehema. Ni haki kwa sisi sote kumtakia rehema midhali atamuhimidi Allaah. Imepokelewa katika Hadiyth isemayo:

“Atapochemua mmoja wenu ambapo akamhimidi Allaah, basi ni haki kwa mwenye kumsikia amtakie rehema.”

Au Hadiyth yenye maana kama hiyo.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ijaabatu as-Saa-il, uk. 401
  • Imechapishwa: 06/09/2019