Tofauti kati ya Takfiyr kwa aina na Takfiyr kwa mtu

Swali: Ambaye anasema kuwa Qur-aan imeumbwa anakufuru?

Jibu: Salaf wamemkufurisha yule mwenye kusema kuwa maneno ya Allaah yameumbwa. Lakini huu ni ukufurishaji wa aina na si kwa mtu kwa dhati yake. Kwa mfano haifai kusema kuwa az-Zamakhshariy alikuwa kafiri kwa sababu alikuwa Mu´taziliy na Mu´tazilah wanasema kuwa Qur-aan imeumbwa. Hata hivyo maoni haya ni kufuru. Kuna tofauti kati ya Takfiyr kwa aina na kwa sifa na kwa mtu. Kwa sababu kumkufurisha mtu kwa dhati yake kunahitajia kutimia kwa vigezo na kuondoka kwa vikwazo.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-Kariym bin ´Abdillaah al-Khudhwayr
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.khudheir.com/audio/2596
  • Imechapishwa: 13/12/2020