Tofauti kati ya Tabdiy´ yenye kuenea na Tabdiy´ maalum

Kuna tofauti kati ya Tabdiy´ iliyoachiwa na yenye kuenea na Tabdiy´ maalum.

Mfano wa Tabdiy´ iliyoachiwa na yenye kuenea ni pale tunaposema kuwa mwenye kusema kuwa matamshi ya Qur-aan yameumbwa ni mtu wa Bid´ah. Hii ni Tabdiy´ kwa njia iliyoenea na kuachiwa.

Mfano wa Tabdiy´ kwa njia maalum ni kama kusema mtu fulani anasema kuwa matamshi ya Qur-aan yameumbwa na kwa ajili hiyo ni mtu wa Bid´ah.

Tofauti kati ya hayo mawili ni kuwa Tabdiy´ ambayo haikufungamana na iliyoenea haina neno na si khatari. Tunasema mwenye kusema kitu fulani ni mzushi. Hata hivyo hatukumlenga mtu. Hii ndio Tabdiy´ iliyoachwa.

Kuhusu Tabdiy´ maalum asli ni kuwa imekatazwa. Haifai kwetu kusema mtu fulani ni mzushi mpaka asimamikiwe na haki. Ataposimamikiwa na haki halafu akaikataa, hapo ndipo itafaa kusema kuwa ni mzushi. Hivyo ndivyo anavyohukumiwa mtu. Kwa sababu mtu anaweza kuwa amefahamu kimakosa kitu fulani, anaweza kuwa mjinga. Atapoangaziwa na akafanya inadi, hapo ndipo itajulikana kuwa ameridhia Bid´ah hii. Katika hali hii itafaa kumfanyia Tabdiy´.

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas Aal ´Abdil-Kariym
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Jarh wat-Ta´diyl ´indas-Salaf, uk. 49-50
  • Imechapishwa: 09/08/2020