Tofauti kati ya mwenye maradhi yenye kuendelea yanayotarajiwa kupona na aliye na maradhi yasiyotarajiwa kupona

Swali: Mgonjwa mwenye maradhi yenye kuendelea afanye nini?

Jibu: Ikiwa mgonjwa maradhi yake ni yale yenye kutarajiwa kupona basi anatakiwa kulipa zile siku zilizompita katikati ya maradhi yake. Lakini akiwa na maradhi yasiyotarajiwa kupona basi anatakiwa kulisha kwa kila siku moja masikini. Robo pishi ya ngano au nusu pishi ya kitu kingine. Ikiwa daktari atamwambia kwamba kufunga wakati wa majira ya joto kunamdhuru. Basi tunamwambia afunge wakati wa majira ya baridi. Huyu hali yake inatofautiana na ya yule ambaye kufunga kunamdhuru siku zote.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/121)
  • Imechapishwa: 19/06/2017