´Aqiydah yetu ni yenye kuafikiana na yenye kudhibiti, ´Aqiydah yao ni yenye kugongana na yenye kutofautiana.

Wanasema kuwa Muusa aliyasikia maneno ya Allaah kutoka kwa Allaah pasi na mkatikati. Kisha wanasema kuwa maneno ni maana kwenye nafsi Yake na sio sauti yenye kudhihiri kihisia.

Wanawaraddi Mu´tazilah wanaosema kuwa Qur-aan imeumbwa. Halafu wanasema kama wanavosema kwamba Qur-aan imeumbwa.

Wanasema kuwa Allaah yuhai, yupo na kwamba ataonekana siku ya Qiyaamah. Halafu wanasema kwamba hayuko juu ya mbingu, juu, chini, kuliani wala kushotoni. Wala haiingii akilini kwamba yupo kwa njia kama hii.

  • Mhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Burhaan fiy Bayaan-il-Qur-aan, uk. 92
  • Imechapishwa: 12/03/2019