Thawabu za mgonjwa anayeswali kwa kukaa ni sawa na mwenye kusimama?


Swali: Mgonjwa akiswali swalah za faradhi kwa kukaa kwa sababu daktari ndiye kamwandikia hivo anapata sawa na yule mwenye kusimama?

Jibu: Akikaa wakati wa kuswali kwa sababu ya udhuru wa maradhi au daktari ndiye kamwelekeza hivo na kwamba kusimama kunamdhuru, basi anapata thawabu sawa na mwenye kusimama. Kwa sababu ameacha kusimama kwa sababu ya udhuru. Kwa hivyo anapata thawabu sawa na mwenye kusimama.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ´alaa al-Hawaa´ http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/09-03-1436.mp3
  • Imechapishwa: 03/12/2017