Swali: Mimi naitwa ´Abdul-Qaadir ambaye nin miaka 25. Nataka kuoa mwanamke mkristo ambaye naye ana miaka 25. Nimemuahidi ya kwamba pale atapoingia katika Uislamu tu basi nitamuoa, jambo ambalo amelifanya. Je, nimuoe? Lakini hata hivyo baba yangu ni mpinzani mkubwa wa ndoa hii.

Jibu: Mambo yakiwa kama ulivosema basi tekeleza ahadi yako kwa huyo mwanamke uliyemtaja; muoe. Upinzani wa baba yako juu ya ndoa hii hauzingatiwi.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (18/09)
  • Imechapishwa: 11/06/2017