Swali: Baadhi ya vijana walienda kwao wakawanasihi na kuwaelekeza walinganie katika Tawhiyd ambapo wakatukasirikia, wakatuhuzunikia na vifua vyao vikaingiwa na chuki dhidi yetu. Je, tubaki pamoja nao au tuwaache?

Jibu: Wafunzwe na wanasihiwe. Tawhiyd inatakiwa ije mwanzo. Ikiwa waislamu wako juu ya Tawhiyd basi wanatakiwa kufunzwa yale wasiyoyajua katika swalah zao na swawm zao. Lakini kati yao kukiwa kuna watu wenye shirki basi wanatakiwa kuanza kwa Tawhiyd. Wanatakiwa kuwafunza Tawhiyd kwanza kwa sababu matendo hayasihi isipokuwa baada ya kusalimika kutokamana na shirki. Lakini wakiwa katika jamii mfano wa hii ya kisaudi na mfano wake – wako katika jamii ya kiislamu nzuri – basi wanatakiwa kuwalingania katika yale wanayodhani kuwa wameyafanyia upungufu, yamejificha kwao na wawazindue kwayo wakiwa ni watu wa Tawhiyd na yale mambo ambayo yamejificha kwao yanayohusiana na swalah zao, swawm zao, zakaah zao, hajj zao na biashara zao. Ama wakiwa kati ya watu makafiri basi wanatakiwa kuanza kwa Tawhiyd na wawatahadharishe shirki.

Swali: Wanasema kuwa sisi tunawafanya watu kukimbia mbali nao?

Jibu: Kulingania katika Tawhiyd sio kukimbiza watu ikiwa ni katika jamii ilio na shirki. Huo ndio ulinganizi wa Mitume ambapo walianza kulingania katika Tawhiyd. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alianza kulingania katika Tawhiyd. Alitumia muda wa miaka kumi yote akilingania katika Tawhiyd kabla ya kufaradhishwa swalah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21521/ما-كيفية-الدعوة-الصحيحة-لفىة-الشباب
  • Imechapishwa: 21/08/2022