Tarehe 27 ndio usiku wenye matarajio makubwa zaidi

Swali: Katika zile siku kumi za mwisho za Ramadhaan tarehe ishirini na saba msikiti Mtakatifu wote wa Makkah watu hujaa na baada ya siku hiyo watu wanaondoka. Wengi wana imani kwamba usiku huo ndio usiku wa Qadr.

Jibu: Ndio usiku wenye matarajio zaidi, kama alivosema Ubayy. Alikuwa akiuapia kwamba ndio usiku wa Qadr.

Mwanafunzi: Baadhi ya watu hupupia kufanya ´Umrah kunako usiku huu.

Ibn Baaz: Inatakikana kwa mtu asijikakame na wala asiwaudhi watu. Afanye ´Umrah katika Ramadhaan na kufanya hivo inatosha. Ni mamoja iwe mwanzoni, katikati au mwishoni mwake. Asijikakame katika usiku huu. Watu wakijikakama kutakuwa na ugumu na uzito kwa wengine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaad-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/23775/هل-يصح-تعيين-ليلة-القدر-بليلة-سبع-وعشرين
  • Imechapishwa: 14/05/2020