Talaka ya yule aliyetalikiwa na mumewe akaolewa kisha akarudi tena mara ya pili


Swali: Mume akimtaliki mke wake halafu akaolewa na mwingine, kisha akamtaliki mume huyo akarudi kwa yule mume wa kwanza. Je, Talaka ya kwanza inahesabika?

Jibu: Akimtaliki Talaka chini ya tatu na akatoka ndani ya eda, akiolewa na mume mwingine akamtaliki kisha akarejea kwa wa kwanza, anarejea kwa hesabu ya Talaka alizobaki nazo na inahesabika ile ya kwanza.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/ar/node/10040
  • Imechapishwa: 08/02/2018