Takfiyr ya ´Ubayd al-Jaabiriy kwa Huuthiyyuun


Swali: Je, Huuthiyyuun Yemen wote ni Raafidhwah au kuko ambao ni Zaydiyyah? Mimi nimewasikia wanachuoni wakisema kuwa Huuthiyyuun ni makafiri na hilo likawa nimenitatiza.

Jibu: Ametakasika Allaah! Mwenye kushuku juu ya ukafiri wa Huuthiyyuun, hali ya kuwa amefikiwa na dalili, ni kafiri. Asiyemkufurisha kafiri anakufuru. Maana yake ni kwamba ikijulikana kuwa mtu fulani ni kafiri na akajua hili pasi na kumkufurisha, basi na yeye ni kafiri kama wao.

Huuthiyyuun ukafiri wao unajulikana na watu wote. Hata wazee wa kike wa kiyemen wanajua ukafiri wao. Tusemeje juu ya wenye busara? Wanafunzi? Wanachuoni? Wanachuoni wamebainisha hili mara nyingi kabisa.

Hivi kwani hamjui kuwa hata kama miili yao iko Yemen lakini mioyo yao iko Iran? Ninasema hili pasi na mashaka.

Raafidhwiy aliyeko al-Madiynah mwili wake uko pamoja na sisi hapa lakini moyo wake uko pamona na Raafidhwah wenzake Iran au ´Iraaq.

  • Mhusika: Shaykh ´Ubayd bin ´Abdillaah al-Jaabiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://ar.miraath.net/fatwah/11320
  • Imechapishwa: 20/09/2020