Swali: Kuhusiana na yaliyowekwa katika Shari´ah wakati wa kumzika maiti wako watu ambao wanasema “Allaahu Akbar” na “Laa ilaaha illa Allaah” kwa wingi pale maiti anaposhuhwa ndani ya kaburi.

Jibu: Hili halina dalili na waka hakukupokelewa kitu kuhusiana na haya. Lakini anachotakiwa mtu ni kushiriki katika kumzika maiti, kuhudhuria kule kuzikwa kwake, kumsindikiza na asimame karibu na kaburi lake wakati wa kuzika na kumuombea msamaha na amuombee kwa Allaah uthabiti wakati wa kuhojiwa. Haya ndio yaliyowekwa katika Shari´ah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ´alaa al-Hawaa´ http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/1436-03-02.mp3
  • Imechapishwa: 03/12/2017