Tahiyyat-ul-Masjid kwa anayekariri kutoka na kuingia msikitini

Swali: Lau mtu atataka kutoka nje ya msikiti kwa sababu ya kitu kilichojitokeza na alikuwa amekaa msikitini, je, ni sunnah kila wakati ataporudi kuswali Rak´ah mbili za Tahiyyat-ul-Masjid?

Jibu: Wanachuoni wametaja kwamba ikiwa kutoka kwake kutajikariri basi ataswali katika ile mara ya mwisho atapoingia. Mfano wa hali hii, kama walivosema wanachuoni, ni kama wanaowajibisha Ihraam kwa yule mwenye kuingia Makkah. Wamesema kwamba yule ambaye anakariri kuingia Makkah kama mkata kuni au afande si lazima kwake kufanya Ihraam kila mara. Lakini ni lazima kwake ile mara ya mwisho.

Maoni ya sawa ni kwamba Ihraam si lazima isipokuwa kwa yule anayetaka kufanya hajj au ´umrah. Kadhalika ambaye kutoka kwake nje ya msikiti kutakariri; hatoswali kila mara. Lakini ile mara ya mwisho ataswali Rak´ah mbili.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (13) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191589#219913
  • Imechapishwa: 25/10/2019