Swawm ya mfungaji anayekabiliwa na moshi mwingi

Swali: Katika kijiji chetu kuna mtu anayefanya kazi ya kutengeneza mikate kwenye mashine ya oveni na ni mtu ambaye anaswali na anafunga Ramadhaan. Ameniuliza kama inafaa kula katika Ramadhaan kwa kuzingatia kwamba anakabiliwa na joto la moto mkali kwa masaa mengi mchana akiwa amefunga?

Jibu: Haijuzu kwa mtu huyo kula. Bali ni lazima kwake kufunga. Kitendo cha yeye kuchoma mikate mchana wa Ramadhaan sio udhuru wa kutofunga. Afanye kazi kadri na awezavyo.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy

´Abdullaah al-Ghudayyaan

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daa’imah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Ladjnah ad-Daa’imah (13489)
  • Imechapishwa: 27/04/2020