Swawm pia inaingia


Swali: Watu wengi wanafunga kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa zile siku kumi. Je, kuna dalili inayothibitisha jambo hilo?

Ibn Baaz:

“Hakuna masiku ambayo matendo mema yanapendwa zaidi na Allaah ndani yake kama masiku haya kumi.”

Je, umeisikia Hadiyth hii?

Mwanafunzi: Ndio.

Ibn Baaz: Je, kufunga ni katika matendo mema au si katika matendo mema?

Mwanafunzi: Ndio.

Ibn Baaz: Basi inaingia pia.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21833/ما-الدليل-على-فضل-صيام-عشر-ذي-الحجة
  • Imechapishwa: 08/07/2021