Swali 08: Ni ipi hukumu ya jeneza linaletwa msikitini na watu wakaswali swalah ya faradhi kuielekea?

Jibu: Sijui makatazo yoyote juu ya hayo. Kilichokatazwa ni kuliekea kaburi na si kumwelekea maiti. Sa´d bin Abiy Waqqaas aliletwa kwa ´Aaishah ili amswalie. Pia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimswalia Ibn Baydhwaa´ msikitini. Kwa hivyo sijui makatazo yoyote juu ya hilo. Wala hatuifisidi swalah.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tuhfat-ul-Mujiyb, uk. 107
  • Imechapishwa: 25/12/2019