Je, swalah ya maamuma inaharibika kwa kuharibika swalah ya imamu?


Swali: Je, swalah ya maamuma inaharibika kwa kuharibika swalah ya imamu?

Jibu: Swalah ya maamuma haiharibiki kwa kuharibika swalah ya imamu. Kwa kuwa swalah ya maamuma ni sahihi. Msingi ni ule usahihi kubaki. Swalah yao haiwezi kubatilika isipokuwa kwa kuwepo dalili sahihi. Imamu swalah yake imebatilika kwa sababu ya dalili sahihi iliyopelekea katika hilo. Maamuma ameingia ndani ya swalah kwa amri ya Allaah na hivyo swalah yake haiwezi kuharibika isipokuwa kwa amri ya Allaah. Kuna kanuni inayosema:

“Mwenye kuingia katika ´ibaadah kwa mujibu wa vile alivyoamrishwa basi sisi hatuwezi kuibatilisha isipokuwa kwa kuwepo dalili.”

Yanavuliwa katika hayo yale yanayosimama nafasi ya maamuma kama mfano wa Sutrah. Sutrah ya imamu ni Sutrah ya wale walio nyuma yake. Mtu akipita kati ya Sutrah ya imamu na Sutrah yake basi swalah ya imamu inaharibika na swalah ya maamuma vilevile inaharibika. Sutrah hii ni yenye kushirikiana. Kwa ajili hii ndio maana hatumuamrishi maamuma kuweka Sutrah. Iwapo ataweka Sutrah itazingatiwa kuwa ni Bid´ah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/451-452)
  • Imechapishwa: 07/08/2017