Swali 358: Tumesikia kuhusu swalah ya haja na swalah ya kuhifadhi Qur-aan. Je, zipo swalah mbili hizi au hazipo?

Jibu: Zote mbili si sahihi. Si hiyo swalah ya haja wala swalah ya kuhifadhi Qur-aan. Kwa sababu mfano wa ´ibaadah hizi haiwezekani kuzithibitisha isipokuwa kwa dalili ya Kishari´ah ambayo ni hoja, jambo ambalo hakuna. Kwa hivyo hazikuwekwa katika Shari´ah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Mar´ah al-Muslimah, uk. 139
  • Imechapishwa: 29/09/2019