Swali 16: Baadhi ya watu wanamkaripia yule anayeswali bila ya kilemba. Ni ipi dalili inayokataza? Je, kuvaa kilemba ni Sunnah au hapana?

Jibu: Kilemba kinazingatiwa ni miongoni mwa zile ada za waarabu ambazo zilikubaliwa na Uislamu. Kusema kwamba kilemba kinafikia kiwango cha Sunnah hakifikii kiwango cha Sunnah. Kinazingatiwa ni ada. Lakini mtu akinuia kumuigiliza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) basi analipwa thawabu kwa kumuigiliza Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Ama kuswali pasi na kilemba ni sahihi. Haitakikani kumkemea mtu anayeswali pasi na kilemba. Haifai kumkemea yeyote isipokuwa kwa dalili kutoka katika Qur-aan na Sunnah. Tunachowanasihi watu ni kuvaa kilemba ndani ya swalah na nje ya swalah. Lakini iwapo atatoka mtu kichwa chake kikiwa wazi asikaripiwe. Hatusemi kuwa swalah yake ni batili.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tuhfat-ul-Mujiyb, uk. 138
  • Imechapishwa: 24/12/2019