Swalah isiyokuwa na unyenyekevu


Swali: Ni ipi hukumu ya unyenyekevu ( الخشوع) katika swalah?

Jibu: Unyenyekevu ndio ubongo wa swalah. Swalah isiyokuwa na unyenyekevu ni kama kiwiliwili kisichokuwa na roho. Kimsingi unyenyekevu unakuwa moyoni kisha ndipo viungo vya mwili vinafuatia kwa utulivu. Kwa msemo mwingine utulivu wa moyo na kumwelekea kwake Allaah (´Azza wa Jall). Tunamuomba Allaah atujaalie kuwa miongoni mwa wanyenyekevu.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (05) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191110#219240
  • Imechapishwa: 22/09/2018