Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“… Swadaqah inazima madhambi kama vile maji yanavyozima moto.”

swadaqah kwa aina zake mbali mbali inafuta madhambi. Haijalishi kitu sawa ikiwa ni swadaqah kwa maneno, matendo ya wajibu na yaliyopendekezwa. Vilevile swadaqah ya mali. Zote hizi zinafuta madhambi kwa kuwa ni matendo mema. Allaah (Jalla wa ´Aaa) Amesema:

إِنَّ الْحَسَنَاتِ يُذْهِبْنَ السَّيِّئَاتِ

“Hakika mema yanaondosha maovu.” (11:114)

Isitoshe tumebainisha maana ya maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mche Allaah popote pale ulipo, fuatisha kitendo kiovu kwa kitendo kizuri kitafuta [kitendo kiovu] na ishi na watu kwa uzuri.”

Ukifahamu maana ya swadaqah ya jumla, basi kila pale ambapo utapitikiwa na dhambi, basi ni juu yake kutoa swadaqah sana. Madhambi hayahesabiki. Kwa kuwa hakuna hali yoyote ile utayokuwemo, isipokuwa Allaah ima amekuamrisha au amekukataza [jambo] katika hali hiyo. Ni wachache wenye kutekeleza maamrisho na makatazo katika hali zote. Kwa hivyo, ni lazima mtu kukithirisha kutoa swadaqah kwa wingi. Swadaqah ni milango ya kheri.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 407
  • Imechapishwa: 14/05/2020