Suruuriyyah na al-Ikhwaan al-Muslimuun ni katika Ahl-us-Sunnah?


Swali: Haya mapote ya leo kama al-Ikhwaan, an-Nahdhwah na as-Suruuriyyah na mengineyo yanahesabika ni katika mapote yaliyotoka katika kundi la waislamu, Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah au ni katika pote lililookoka, al-Firqat-un-Naajiyah na kuwepo kwake ni Kishari´ah na wanaowapa bay´ah ni katika Ahl-us-Sunnah?

Jibu: Ama mapote haya na mengineyo hayahesabiki kuwa ni katika Ahl-us-Sunnah. Kilichobaki ni hukumu ya mmoja kwa mmoja. Hatuwezi kuhukumu moja kwa moja kwa mtu binafsi ya kwamba ametoka katika al-Firqat-un-Naajiyah. Huenda akawa ni mjinga na hajui. Yule anayejua Da´wah ya al-Ikhwaan al-Muslimuun, Suruuriyyah na makundi mengine ambayo yanakwenda kinyume na Sunnah na akalingania kwayo na akawa na Ta´assub juu yake, huyu tunaweza kusema ya kwamba sio katika al-Firqat-un-Naajiyah.