Sunnah kwa imamu na waswaliji baada ya kumaliza kuswali

Swali: Mwenye kusema kabla ya kugeuka au kukunja miguu yake, kama ilivyokuja katika Hadiyth:

لا إله إلا الله وحده لا شريك له، له الملك وله الحمد وهو على كل شيء قدير بعد المغرب والفجر

“Hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, hali ya kuwa yupekee hana mshirika, ufalme ni Wake, himdi ni Zake, Naye juu ya kila jambo ni muweza” baada ya Maghrib na Fajr… “ mpaka mwisho wa Hadiyth.

Hadiyth nyingine iliyopokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) isemayo kwamba alikuwa akigeuka baada ya kusema:

اللهم أنت السلام

“Ee Allaah! Wewe ndiye as-Salaam.

Je, haya ni mambo yanayofanywa na imamu tu au ni pamoja vilevile na maamuma na yule anayeswali peke yake?

Jibu: Kuhusu imamu hatakiwi kubaki anaelekea Qiblah isipokuwa kwa kiwango cha kusema “Astaghfir Allaah” mara tatu na kusema vilevile:

واللهم أنت السلام ومنك السلام تباركت يا ذا الجلال والإكرام

“Ee Allaah! Wewe ndiye as-Salaam, amani inatoka Kwako, umebarikika, Ee Mwenye utukufu na ukarimu.”

Baada ya imamu kusema:

Astaghfir Allaah! Astaghfir Allaah! Astaghfir Allaah!”

واللهم أنت السلام ومنك السلام تباركت يا ذا الجلال والإكرام

“Ee Allaah! Wewe ndiye as-Salaam, amani inatoka Kwako, umebarikika, Ee Mwenye utukufu na ukarimu.”

ageuke. Hivo ni kwa kuwa maamuma wamefungamana na yeye. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Msimtangulie kugeuka.”

Ikiwa maamuma wamefungamana na yeye basi haitakiwi kwake kubaki akawa hivo hali amewatia regezani. Aseme kwa kiwango vile Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema kisha ageuke. Hii ndio Sunnah kwa imamu.

Kuhusu maamuma imamu akishageuka na wao wanaweza kugeuka. Kuhusu yaliyokuja katika Hadiyth:

“… kabla ya kukunja miguu yake.”

maana yake ni kwamba aseme hivo na bado yuko sehemu yake. Ni mamoja akakunja miguu yake kwa kufuata Sunnah kama imamu au asikunje.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (36) http://binothaimeen.net/content/808
  • Imechapishwa: 30/05/2020