Soksi mbili na kufuta juu yake


Swali: Kuna mtu amefuta juu ya soksi kisha akavaa soksi zengine ilihali bado yuko na wudhuu´. Je, afute juu yake?

Jibu: Akivaa soksi akafuta juu yake kisha akazivua na akavaa zengine, tutatazama; ikiwa amezivaa baada ya kufuta zile za kwanza asifute zile zengine. Ama ikiwa amevua zile soksi za kwanza kabla ya kupangusa juu yake bali yuko na twahara yake kisha akabadilisha soksi, hapa muda utaanza kuhesabiwa baada ya ule mpanguso wa mara ya kwanza baada ya kupatwa na hadathi. Lau mtu atavaa soksi na akapangusa juu yake kisha akaona kuwa ni mwenye kuhitajia soksi zengine ambapo akavaa soksi zengine akiwa na twahara ya ufutaji wa kwanza, hapa hakuna neno katika hilo. Muda unaanza kuanzia pale atapofuta zile za kwanza na sio zile za pili.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (77) http://binothaimeen.net/content/1766
  • Imechapishwa: 14/09/2020