Siwaak inatumiwa kabla au katikati ya wudhuu´?

Swali: Ni Sunnah kutumia Siwaak kabla ya wudhuu´ au katikati ya wudhuu´?

Jibu: Kabla ya wudhuu´. Hadiyth inasema:

”…. wakati wa kila wudhuu´.”

Swali: Sunnah ni kutumia Siwaak kwa mkono wa kulia au wa kushoto?

Jibu: Sunnah ni kutumia Siwaak kwa mkono wa kushoto kwa kuwa inahusiana na kuondosha uchafu kinywani na kwenye meno. Hayo yanafanywa kwa mkono wa kushoto.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (5) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdt–01041434.mp3
  • Imechapishwa: 09/10/2016