Kuhusiana na mambo ya kidunia, sisi si katika wale wanaojali sana hilo na kuyatafuta. Tuna uadui mwingi na wengi miongoni mwa watu wa Bid´ah. Lau tungelikuwa kama Msudani Muhammad Haashim al-Hadiyyah na tukataka mali, tungelienda kwa Masufi na kusifu Usufi wake, pia hali kadhalika Mashia, Hizbiyyuun na wengine ili wawe radhi nasi. Lakini mikanda yetu na vitabu vyetu vimejaa Radd kwa watu wa Bid´ah na Hizbiyyuun. Lau ingelikuwa sisi tumemuingilia ´Abdur-Rahmaan ´Abdul-Khaaliq peke yake, mtu angeliweza kusema hivyo. Lakini ´Abdur-Rahmaan ´Abdul-Khaaliq ni mmoja katika Hizbiyyuun na watu wa Bid´ah ambaye tunawatahadharisha watu naye kwa kutafuta ujira na thawabu.

Shu´bah aliwaambia marafiki zake:

”Njooni! Wacha nisengenye kwa ajili ya Allaah.”

Imaam Ahmad pia anasema:

”Mtu anayewapiga Radd watu wa Bid´ah ni kama mpiganaji Jihaad.”

Hali kadhalika amesema hivyo Shaykh-ul-Islaam bin Taymiyyah (Rahimahu Allaah).

Makusudio yetu tunatafuta ujira na thawabu.

  • Mfasiri: Firqatunnajia.com