Swali: Una nasaha gani kwa maimamu wa misikiti ambao haraka tu baada ya kumaliza al-Faatihah wanasoma Suurah nyingine na hawawapi maimamu fursa ya kusoma al-Faatihah?

Jibu: Si lazima kwa imamu kuwasubiri waswaliji kusoma al-Faatihah. Anapomaliza kusoma al-Faatihah basi inafaa kwake kusoma Suurah nyingine hata kama hakuwasubiri. Waswaliji wakiweza kusoma katika kile kinyamazo cha imamu wafanye hivo. Wakisoma kimyakimya pia ni sawa. Ana khiyari kati ya kusikiliza kisomo cha imamu au kusoma al-Faatihah. Akisikiliza kisomo cha imamu ni kisomo chake na akiweza kusoma al-Faatihah ni vyema na asizidishe juu yake kitu kingine.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.mufti.af.org.sa/ar/content/فتاوى-على-الهواء-26-12-1435هـ
  • Imechapishwa: 19/06/2022