Si ingelikuwa bora Tarawiyh iswaliwe kwenye msikiti mmoja mkubwa?

Swali: Je, lililo bora ni swalah ya Tarawiyh kuswaliwa kwenye kila msikiti au baadhi ya misikiti ijikusanye kama mfano iwe katika msikiti mmoja mkubwa ili kuwepo mkusanyiko mkubwa na uchangamfu zaidi?

Jibu: Kinachonidhihirikia ni kwamba watu wafanyiwe wepesi na kwamba watu wabaki katika vitongoji vyao na kwamba kila kitongoji kiswali Tarawiyh katika msikiti wao ili nyumba za Allaah ziimarishwe kwa waswaliji. Jengine ni kwamba iwapo tutasema kuwa wakusanyike katika msikiti mmoja kitendo hicho kitapelekea kususwa misikiti mingine na misikiti mingine itabanwa. Nyinyi wenyewe mnajua hivi sasa kwamba mambo si kama ilivyokuwa zamani. Leo watu wanakuja na magari ambapo kila mmoja anakuja na gari lake. Matokeo yake kutatokea kubanana na tabu. Vile ninavyoona ni kwamba swalah ya Tarawiyh iswaliwe kwenye misikiti kama zinavoswaliwa swalah za faradhi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (70) http://binothaimeen.net/content/1591
  • Imechapishwa: 14/03/2020