Swali: Maneno Yake (Ta´ala):

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ

“Hakika Allaah hasamehi kushirikishwa na anasamehe yaliyo chini ya hayo kwa Amtakae.”[1]

Je, ndani yake kunaingia shirki ndogo? Ni ipi tafsiri ya ´shirki ndogo`?

Jibu: Kuna wanachuoni waliosema kuwa shirki ndogo inaingia ndani ya shirki kubwa kutokamana na ujumla wa Aayah na vilevile wamefanya hivo kuiheshimu Qur-aan. Maana ya:

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ

“Hakika Allaah hasamehi kushirikishwa na anasamehe yaliyo chini ya hayo kwa Amtakae.”

ni kwamba shirki kubwa mwenye nayo atakuwa ni mwenye kudumishwa Motoni milele.

Ama kuhusu shirki ndogo ni yenye kukabiliana na matendo mema. Ikiwa matendo mema ya mtu ndio mengi basi yanaifuta shirki [ndogo] hii na mwenye nayo anaingia Peponi. Ikiwa matendo maovu ya mtu ndio mengi basi mwenye nayo ataadhibiwa Motoni kwa shirki hii ndogo.

Kuhusu mtu ambaye ana dhambi kubwa yuko chini ya utashi wa Allaah; Allaah anaweza kumsamehe na wala asiyafute maovu yake kwa mema yake kama ambavyo vilevile anaweza kumuadhibu Motoni. Kuna wanachuoni wengine wamesema vilevile ya kwamba shirki ndogo ni kama dhambi kubwa.

[1] 04:48

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (01) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=190884#219018
  • Imechapishwa: 29/12/2017