Sherehe baada ya kukhitimisha Qur-aan katika Tarawiyh

Swali: Baadhi ya watu katika baadhi ya misikiti wamezowea kufanya karamu ya chakula kwa ajili ya waswaliji baada ya kumaliza Qur-aan yote katika swalah ya Tarawiyh. Ni ipi hukumu ya karamu hii na kuhudhuria?

Jibu: Karamu hii iliyotajwa haina dalili kutoka katika Sunnah. Kwa hivyo bora ni kuacha kufanya hivo.

´Abdul-´Aziyz Aalish-Shaykh

Swaalih al-Fawzaan

´Abdullaah al-Ghudayyaan

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah nr. (21787)
  • Imechapishwa: 23/04/2022