Shaytwaan amewapendezeshea watu picha

Swali: Watu wengi wamechukulia sahali suala la picha na khaswa video na simu. Baadhi ya wanaofanya hivo udhahiri wao ni wema. Ni ipi nasaha yako?

Jibu: Bila ya sahaka hii ni katika fitina. Shaytwaan siku zote anawatingisa watu katika fitina na anawaletea kitu cha khatari ili kuwadanganya watu kwacho. Haya ni katika matendo ya shaytwaan. Watu kujishughulisha na mambo ya picha na kughafilika kwayo na uharamu wake na adhabu yake, shaytwaan amewapendezeshea nayo.

Lililo la wajibu ni kuzinduka kwa jambo hili. Mtu hana haja ya picha.

Kuhusiana na akilazimika kuchukua picha, wanachuoni wamefutu kiasi cha dharurah kama mfano wa picha ya kitambulisho, pasipoti, picha kwa ajili ya kutaka kumjua aliyetenda tendo la jinai n.k. Haya ni mambo ya kidharurah. Yasiyokuwa haya hakuna haja nayo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (06) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2121
  • Imechapishwa: 02/07/2020