Swali: Siku za nyuma wanakuja wanawake wengi na camera na kuwachukua picha walioko Haram. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Ni haramu na haijuzu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewalaani watengeneza picha na akasema kuwa ndio watu wataokuwa na adhabu kali siku ya Qiyaamah. Amesema pia:

“Allaah (Ta´ala) amesema: “Ni nani dhalimu mkubwa kuliko yule ambaye anajaribu kuumba mfano wa viumbe Wangu? Hebu waumbe mdudu chungu, waumbe punje ya nafaka au waumbe chembe ya shayiri.”[1]

Bi maana wenye kufanya picha.

Haijuzu kwa wanamme wala wanawake kuchukua picha Haram wala kwenginepo. Ingawa Haram ni kubaya zaidi kwa sababu madhambi yanayofanywa mahali hapo yanapewa uzito zaidi. Picha hazifai mahali kokote, moja kwa moja, lakini Haram ni kubaya zaidi:

وَمَن يُرِدْ فِيهِ بِإِلْحَادٍ بِظُلْمٍ نُّذِقْهُ مِنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ

”Na yeyote anayekusudia humo kufanya upotofu kwa dhulma Tutamuonjesha adhabu iumizayo.” (22:25)

Mtu anaadhibiwa kwa kuweka tu ile nia ya dhambi – tusemeje ikiwa ataitenda? Haijuzu. Ni lazima kwa yule mwanamme na mwanamke anayefanya hivo atubu kwa Allaah, aache kuchukua picha na aziharibu picha na camera. Camera ni haramu na haijuzu kuibakiza.

[1] al-Bukhaariy (5953) na (7559) na Muslim (2111).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=2UxCYbdCtxw
  • Imechapishwa: 07/07/2022