Swali 185: Ni ipi hukumu ya kuwapa pesa nyingi makafiri?

Jibu: Hakuna neno ikiwa katika kufanya hivo kuna manufaa kwa waislamu kwa ajili ya kuepuka shari yao. Hata zakaah wanapewa sehemu yake wale makafiri ambao zinataka kulainishwa nyoyo zao kwa ajili ya kuepuka shari yao ya ukafiri. Kafiri ambaye kuna matarajio ya kuiepuka shari yake dhidi ya waislamu anatakiwa kupewa sehemu ya zakaah ambayo ni ya faradhi. Ni vipi asipewe pesa ambayo sio zakaah kwa ajili ya kuepuka madhara yake kwa waislamu? Haya ni miongoni mwa yale ambayo baadhi ya wajinga wanafikiria kuwa ni kujenga urafiki nao. Huku sio kujenga urafiki nao. Huku ni kwa ajili ya kuepuka khatari na shari yao dhidi ya waislamu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ´Ulamaa-ul-Kibaar fiy al-Irhaab wat-Tadmiyr, uk. 377
  • Imechapishwa: 12/01/2020