Salafiyyuun hatukubali matahadharisho kwa watu bila dalili na hoja

Nawanasihi waislamu wote ulimwenguni na khaswakhaswa Salafiyyuun Senegal juu ya kumcha Allaah (´Azza wa Jall) na kumtakasia Yeye nia katika maneno, matendo yao na mienendo yao yote. Msimamo wao wakati wa fitina iwe msimamo wa Salafiyyuun na maimamu wa Uislamu uliosimama juu ya Qur-aan na Sunnah. Katika hayo ni kuthibitisha kwanza wanaposikia matusi kutoka kwa Salafiyyuun na wengineo. Ni lazima kwa mtu kuthibitisha kwanza na kuomba dalili.

Matusi ya leo hii ambayo yamewagawa Salafiyyuun, kuwatawanyisha ni matusi batili na hayakusimama juu ya dalili yoyote. Yamesimama kinyume na mfumo wa Salaf. Huenda wengine wanaona aibu kwa mfano wa usulubu kama huu.

Kwa hiyo mimi nawausia Salafiyyuun Senegal watengeneze udugu kati yao na wasikubali maneno ya yeyote awaye ambaye anawaponda wengine isipokuwa mpaka awe na dalili za waziwazi kabisa na zilizo na ubainifu. Ama kuwatukana wengine pasi na dalili ni dhuluma na hata watu wengi wa Bid´ah hawalikubali hilo. Mcheni Allaah na piteni juu ya mfumo wa as-Salaf as-Swaalih na msikubali matusi kutoka kwa yeyote akiwatukana watu au makundi pasi na dalili wala hoja. Bali ni wajibu kumrudishia mwenyewe hiyo batili yake.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=5kXa8vFEMtY
  • Imechapishwa: 10/09/2018