Swali 190: Wanadai baadhi ya watu kwamba Salafiyyah inazingatiwa ni kundi miongoni mwa makundi yaliyoenea uwanjani na hukumu yake ni hukumu ya makundi mengine. Unasemaje juu ya madai haya?

Jibu: Kundi la Salafiyyah ndio kundi lililo juu ya haki. Ndilo kundi ambalo ni lazima kujiunga nalo, kushirikiana nalo na kujinasibisha nalo. Makundi mengine ni lazima kutoyazingatia kuwa katika makundi ya Da´wah kwa sababu ni yenye kwenda kinyume. Ni vipi utafuata kundi linaloenda kinyume na mwongozo wa wema waliotangulia?

Kundi linalokwenda kinyume na Salafiyyah basi ni lenye kwenda kinyume na mfumo wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na ni lenye kwenda kinyume na yale aliyokuwemo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake.

Msemo wa mwenye kusema kwamba kundi la Salafiyyah lenyewe ni miongoni mwa makundi ya Kiislamu. Msemo huu wa makosa. Kundi la Salafiyyah ndio kundi la kipekee ambalo ni lazima kulifuata, kupita juu ya mwongozo wake, kujiunga nalo, kupambana bega kwa bega pamoja nalo. Makundi mengine haifai kwa muislamu kujiunga nayo. Kwani yenye kwenda kinyume. Hivi kweli mtu ataridhia vipi juu ya wale wenye kwenda kinyume na mfumo wa Salaf? Hakuna muislamu anayeridhia jambo hilo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Jilazimisheni na Sunnah zangu na Sunnah za makhaliyfah wangu waongofu baada yangu.”

Amesema kuhusu kundi lililookoka:

“Ni lile litakalofuata yale ninayofuata mimi hii leo na Maswahabah zangu.”

Hivi kweli mtu atataka kuokoka halafu apite njia ya kinyume?

Unataka uokovu na hufuati njia yake?

hakika safina haipiti nchikavu

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ´Ulamaa-ul-Kibaar fiy al-Irhaab wat-Tadmiyr, uk. 404
  • Imechapishwa: 02/03/2020