Swali: Kumejitokeza kundi linalotaka kuleta umoja kati ya Salafiyyah na al-Ikhwaan al-Muslimuun. Hoja yao wanaona kuwa Salafiyyuun hawana mpangilio na uhalisia, kitu ambacho wao wanataka kukifanya. Je, kundi hili limewekwa katika Shari´ah?

Jibu: Inategemea na wanachokusudia kwa mpangilio huo.

Mimi kama nilivosema mara nyingi kupanga darsa na mikutano kunafanana na shule za kiserikali. Hakuna yeyote anayeona kuwa hayafai. Hakukuwepo shule zozote kipindi cha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam); zimekuja baadaye. Hapana shaka kwamba hilo ni aina fulani ya mpangilio na halikataliwi.

Na kama wanakusudia michakato ya kisiri inayopanga kumfanyia uasi mtawala wa kiislamu, jambo hilo pasi na shaka kwanza halijuzu. Jambo la pili Salafiyyuun wanaojaribu kukusanya ulinganizi wa Salaf na mpangilio wa Khalaf watafeli; hawatokuwa Salafiyyuun wala Ikhwaaniyyuun. Ulinganizi haufaulu mpaka utekelezwe wakati wote. Ni kama yalivyo matendo mengine yote ya kisayansi; inahitaji kutaalumika. Wakati aina fulani ya kitendo inachanganyikana nayo, hakuimariki si kimoja wala kingine.

Hata hivyo mimi daima husema kwamba kila kundi linatakiwa kufanya wajibu wake kwa sharti uwe ni wenye kuafikiana na Qur-aan na Sunnah kwa ufahamu wa Salaf. Mfano wa kutaalumika aina hii haukataliwi, lakini haijuzu kuchanganya kati ya hili la kwanza na la pili. Mudiri hawezi kuwa mwalimu. Kazi yake ni ya idara. Wala mwalimu hawezi kuwa mudiri. Kazi yake yeye ni ya kusomesha. Kile kinachoweza kusemwa juu ya mtu mmojammoja kinaweza pia kusemwa juu ya makundi. Kukiwepo Salafiyyuun wanaotaka kukusanya kati ya kulingania na wawe wamepangiliwa (khaswa ikiwa mpangilio huo haukuwekwa katika Shari´ah), basi watafeli na hawatashinda chochote.

  • Mhusika: Imâm Muhammad Nâsir-ud-Dîn al-Albânî (d. 1420)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Raabigh (7) Muda: 5:15
  • Imechapishwa: 17/08/2021