Salaf walifahamu vyema Aayah hii kuliko Suufiyyah

Swali: Baadhi ya Suufiyyah wanatumia dalili juu ya kujuzu kusherehekea maulidi maneno Yake (Ta´ala):

قُلْ بِفَضْلِ اللَّـهِ وَبِرَحْمَتِهِ فَبِذَٰلِكَ فَلْيَفْرَحُوا هُوَ خَيْرٌ مِّمَّا يَجْمَعُونَ

“Sema: “Kwa fadhilah za Allaah na kwa rehema Zake, basi kwa hayo wafurahi – hayo ni kheri kuliko wanayoyakusanya.”[1]

Jibu: Aayah hii ilisomwa na Maswahabah, Taabi´uun waliisoma na waliokuja baada ya Taabi´uun waliisoma, lakini hawakufahamu ufahamu huo. Ingelikuwa kheri basi wangelitangulia kuyafanya. Wanafurahi kwa kuongozwa katika Uislamu, kuongozwa kuijua haki na uongofu na juu neema hizi kubwa zisizolingana na neema nyingine. Wanafurahi kwa haya. Sio kufurahi kwa jambo lililozuliwa ambalo Allaah hakuliteremshia dalili yoyote. Maswahahabah hawakufahamu kutoka katika Aayah hii ufahamu huu na hivyo wakazua kitu hichi kilichozuliwa katika karne ya nne. Watu waliisoma katika karne zote. Kitu hichi kilichozuliwa na kuvumbuliwa kilijitokeza katika karne ya nne na lau kingelikuwa ni kheri basi wangelitangulia kukifanya Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Taabi´uun na waliokuja baada ya Taabi´uun.

[1] 10:58

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bid´at-ul-Mawaalid wa mahabbat-in-Nabiyy http://www.ajurry.com/vb/showthread.php?t=36078
  • Imechapishwa: 07/11/2019