Maswahabah, Taabi´uun na maimamu waliokuja baada yao kabla ya kujitokeza kwa Jahmiyyah, Raafidhwah, Mu´tazilah na Khawaarij wameafikiana juu ya kwamba waumini watamuona Mola Wao kwa macho yao Aakhirah. Bado mpaka hii leo maimamu na Ahl-us-Sunnah wananukuu maafikiano haya. Aliyekuja nyuma anayapokea kutoka kwa aliyetangulia. Aliyetangulia anamrithisha nayo aliyekuja nyuma. Wanathibisha hayo, wanatoa fatwa kwa hayo, wanazungumza hayo kwa marefu na mapana, wanajifakharisha kwayo na kizazi kinarithisha kizazi kingine. Bali wao wanaonelea kuwa neema kubwa kwa Mola Wao ni kwamba watamuona Mola Wao Aakhirah. Nyinyi mnaopinga kuonekana kwa Allaah Aakhirah mmepinga neema kubwa ambayo watapewa watu wa Peponi. Neema hiyo si nyingine bali ni kumuona Allaah.

al-Bayhaqiy (Rahimahu Allaah) amenukuu maafikiano ya Maswahabah juu ya kuthibitisha kuonekana kwa Allaah Aakhirah. (Tazama Haadi al-Arwaah, uk. 233.)

Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah; maimamu na wanachuoni bado wanaendelea mpaka hii leo kuandika vitabu na wanaonelea kuwa yule mwenye kupinga kuonekana kwa Allaah Aakhirah kuwa ni Mu´attwil na ni katika Ahl-ut-Ta´twiyl waovu zaidi.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (01/229-230)
  • Imechapishwa: 30/05/2020