Ni matendo gani ya kheri ya kufanya yaliyokokotezwa katika Ramadhaan?


Swali: Ni matendo gani ya kheri ya kufanya yaliyokokotezwa katika mwezi wa Ramadhaan?

Jibu: Matendo ya kheri ya kufanya yaliyokokotezwa Ramadhaan ni mengi. Muhimu miongoni mwayo:

1- Kuhifadhi kutekeleza yale aliyofaradhisha Allaah katika Ramadhaan na nje ya Ramadhaan kukiwemo swalah na swawm.

2- Baada ya hapo mtu akithirishe kufanya ´ibaadah za Sunnah kukiwemo swalah, tarawiyh, tahajjud, swadaqah na i´tikaaf.

3- Mtu akithirishe kuleta Adhkaar kama kusema “Subhaan Allaah”, “Laa ilaaha illa Allaah” na “Allaahu Akbar”.

4- Kukaa misikitini kwa ajili ya kufanya ´ibaadah ndani yake.

5- Mtu vilevile ailinde swawm yake kutokamana na maneno na matendo vya haramu au vilivyochukizwa ambavyo ima vinaiharibu au kuitia kasoro.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaam al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14891
  • Imechapishwa: 09/06/2017