Rak´ah mbili msikitini wakati uliokatazwa wakati mtu anapofika kutoka safarini

Swali: Mtu ambaye amefika kutoka safarini aswali aswali msikitini katika ule wakati uliokatazwa kuswali ndani yake?

Jibu: Akiingia msikitini aswali ikiwa swalah hiyo ina sababu kama tulivotangulia kusema kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliamrisha kuswali Rak´ah mbili wakati mtu anapofika kutoka safarini. Hivyo akiingia msikitini anakuwa na sababu ya kufanya hivo.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (11) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191491#219817
  • Imechapishwa: 27/05/2019