Swali: Allaah (Ta´ala) amesema:

قُلْ أَبِاللَّـهِ وَآيَاتِهِ وَرَسُولِهِ كُنتُمْ تَسْتَهْزِئُونَ لَا تَعْتَذِرُوا قَدْ كَفَرْتُم بَعْدَ إِيمَانِكُمْ

”Sema: ”Je, mlikuwa mnamfanyia istihizai Allaah na Aayah Zake na Mtume Wake? Hivyo msitoe udhuru, kwani mmekwishakufuru baada ya kuamini kwenu.” (at-Tawbah 09:66)

Je, katika Aayah hii kuna dalili inayofahamisha kwamba kitendo au neno linaweza kumtoa mtu nje ya Uislamu na ndani yake kuna Radd kwa Murji-ah?

Jibu: Ndio, pasi na shaka. Kuna Radd kwa Murji-ah wanaosema kwamba mtu hawezi kukufuru isipokuwa mpaka aamini ndani ya moyo wake. Aayah inafahamisha kwamba mtu anakufuru moja kwa moja. Ni mamoja ameamini ndani ya moyo au hakuamini. Mwenye kufanya mzaha na istihzai hakuamini ndani ya moyo. Pamoja na hivo Allaah amemkafirisha:

قَدْ كَفَرْتُم بَعْدَ إِيمَانِكُمْ

”Mmekwishakufuru baada ya kuamini kwenu.”

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 141
  • Imechapishwa: 23/12/2018