Swali: Ni ipi Radd kwa mwenye kusema kwamba kuigawa Tawhiyd aina tatu ni kujifananisha na wakristo katika imani yao ya utatu?

Jibu: Ulinzi unatafutwa kwa Allaah. Anafananisha ´Aqiydah ya Tawhiyd na imani ya utatu? Haya yamo katika Qur-aan. Aina tatu za Tawhiyd zimechukuliwa kutoka katika Qur-aan. Aayah zote zinazozungumzia juu ya matendo ya Allaah na uwezo Wake ni Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah. Aayah zote zinazozungumzia juu ya kumuabudu Allaah ni Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah. Aayah zote zinazozungumzia juu ya majina na sifa za Allaah ni Tawhiyd-ul-Asmaa´ was-Swifaat. Aina tatu hizi zimetolewa katika Qur-aan. Lakini huyu ima ni mjinga au anajifanya kukosea na vilevile ni mpotevu ambaye analenga kukosea. Haya yanapatikana katika Qur-aan kwa kupitia tafiti za kisomi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (05) http://alfawzan.af.org.sa/node/2048
  • Imechapishwa: 26/11/2016