Radd kwa ad-Daduu kudai kwake kwamba Qur-aan imeumbwa


Swali: Kuna mlinganizi mmoja kwenye TV amesema kuwa kusema kuwa Qur-aan imeumbwa ni kufuru ndogo na amenasibisha maoni hayo kwa Muhammad bin Naswr al-Khuzaa´iy na amesema pia kuwa ni kana kwamba Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amemili katika maoni haya[1].

Jibu: Huyu ni mwongo. Anayesema hivi ni mwongo. Mwenye kusema kuwa Qur-aan imeumbwa anakufuru kufuru kubwa. Allaah amesema kuwa Qur-aan ni maneno Yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuwa Qur-aan ni maneno ya Allaah:

وَإِنْ أَحَدٌ مِّنَ الْمُشْرِكِينَ اسْتَجَارَكَ فَأَجِرْهُ حَتَّىٰ يَسْمَعَ كَلَامَ اللَّـهِ

“Na ikiwa mmoja wa washirikina akikuomba umlinde, basi mlinde mpaka asikie Maneno ya Allaah.” (09:06)

Qur-aan ni maneno ya Allaah na hayakuumbwa. Mwenye kusema kuwa imeumbwa anamkufuru Allaah (´Azza wa Jall) kwa kuwa anamkadhibisha Allaah, Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na maafikiano ya waislamu. Sifikirii kuwa Muhammad bin Naswr al-Khuzaa´iy (Rahimahu Allaah) ana maoni haya. Na kama alifanya hivo ni kosa.

[1] TV ”Iqraa’”, barnamiji ”Fiqh-ul-´Aswr”, 2007-05-08.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (10) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-08-13.mp3
  • Imechapishwa: 12/06/2018