Raafidhwah uongo kwao ni wa tangu kale

Wanachuoni wameafikiana juu ya kwamba Raafidhwah ndio pote warongo kabisa. Uongo kwao ni kitu cha zamani. Ndio maana maimamu wa Uislamu walikuwa wanaweza kuwapambanua kutokana na uongo wao mwingi. Ashhab bin ´Abdil-´Aziyz ameeleza kwamba Maalik aliulizwa kuhusu Raafidhwah. Akasema:

“Usiwaongeleshe na wala usipokee chochote kutoka kwao. Wanasema uongo.”

Harmalah amesimulia kwamba alimsikia ash-Shaafi´iy akisema:

“Sijamuona yeyote akishuhudia uongo kama Raafidhwah.”

Yaziyd bin Haaruun amesema:

“[Hadiyth] ziandikwe kutoka kwa Ahl-ul-Bid´ah midhali mtu halinganii katika Bid´ah zake isipokuwa tu Raafidhwah. Kwani hakika wanasema uongo.”

Shariyk amesema:

“Nachukua Hadiyth kutoka kwa kila ninayekutana naye isipokuwa tu Raafidhwah. Kwani wao wanatunga Hadiyth na wanazichukulia kuwa ni dini.”

al-A´mash amesema:

“Mimi sikudhaminini kwamba hawatosema: “Tumemkuta al-A´mash akiwa na mwanamke.”

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islâm Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Minhaaj-us-Sunnah an-Nabawiyyah (1/59-62)
  • Imechapishwa: 25/12/2018